PEP GUADIOLA AKUMBANA NA KICHAPO CHA HAJA TOKA KWA EVERTON
Pambano la ligi kuu ya soka nchini England kati ya Wenyeji Everton na Manchester City limemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-0.
Kikosi cha kocha Pep Guadiola kilikumbana na kipigo hicho katika mechi ya mapema leo ikiwa ni moja kati ya mechi mbili katika ligi kuu ya England leo.
Romelu Lukaku alitangulia kuipa Everton bao la kuongoza akimalizia pasi ya Kevin Miralas bao lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili ndicho kilichoizamisha zaidi Manchester City kwani magoli matatu yalipatikana katika kipindi hicho Kevin Miralas,Tom Davies na Ademola Lookman.
Matokeo hayo yanaipa Everton pointi 3 muhimu ambazo zinaifikisha pointi 33 katika nafasi ya 7 wakati Manchester City wakibaki nafasi ya 5 na pointi zao 42.

No comments