IBRAHIMOVIC ASAWAZISHA MAKOSA YA POBGA KUINUSURU MAN UNITED NA KICHAPO


Makosa ya mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba kuushika mpira na kusababisha penati iliyozaa goli la kwanza kwa Liverpool yalisawazishwa na Zlatan Ibrahimovic aliyefunga bao la kusawazisha.

Mchezo baina ya Manchester United na Liverpool ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 United wakisawazisha dakika za mwisho za kipindi cha pili.

James Milner ndiye aliyeifungia Liverpool bao kwa njia ya penati kabla ya Zlatan Ibrahimovic hajaisawazishia United dakika ya 84 ya mchezo.

Matokeo hayo yanawafanya Liverpool kufikisha pointi 45 katika nafasi ya 3 sawa na Tottenham wanaoshika nafasi ya pili wakati Manchester United wanabaki katika nafasi ya 6 na point zao 40.

No comments

Powered by Blogger.