MECHI 40 REAL MADRID BILA KUFUNGWA ZAISHIA KWA SEVILLA
Rekodi ya kucheza michezo 40 bila kufungwa kwa Real Madrid imehitimishwa kwa kufungwa bao 2-1 na Sevilla
Mchezo huo wa ligi kuu nchini Spain uliishuhudia Real Madrid ambayo tangu msimu mpya uanze haijapoteza mchezo ikisulubiwa kwa bao la dakika ya mwisho la mshambuliaji mpya wa Sevilla Stefan Jovetic ambaye aliwahi kuichezea Manchestwr City.
Cristiano Ronaldo alitangulia kuipa Real Madrid goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Dan Calvajal kuangushwa na kipa wa Sevilla lakini Nahodha Wa Madrid Sergio Ramos akaisawazishia Sevilla kwa bao la kujifunga kabla ya Jovetic kufanya yake.
Licha ya kufungwa bado Real Madrid wanaendelea kuongoza katika msimano wa ligi hiyo wakiwa na pointi 40 huku Sevilla wakipanda mpaka nafasi ya pili na pointi zao 39.


No comments