MAN UNITED VS LIVERPOOL LEO : HAYA NDIYO MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAJUA
Wapinzani wa jadi katika soka la England Manchester United na Liverpool zitakutana leo katika pambano la marudiano katika ligi kuu ya England baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare.
www.wapendasoka.com tumekuwekea hapa mambo muhimu unayopaswa kuyajua kuelekea katika pambano hilo.
- Hii ni mechi ya 50 baina ya timu hizo katika ligi kuu ya England
- Liverpool imepoteza mechi 11 kati ya mechi 14 baina ya timu hizo katika uwanja wa Old Trafford.
- Hii ni kati ya mechi ambayo lazima magoli yapatikane kwani mara ya mwisho mechi kama hii kumalizika bila magoli yani sare ya bila kufungana ilikua msimu wa mwaka 1919-20 takribani miaka 100 iliyopita.
- Man United Imeshinda mechi 9 zilizopita katika mashindano yote ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 2009 ilipofikisha mechi 11 bila kufungwa.
- Man United kama ikishinda leo itakua imefikisha ushindi wake wa 7 mfululizo katika mechi za ligi pekee ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwezi Januari mpaka Machi 2013.
- Wayne Rooney anahitaji goli moja tu kuweka rekodi mpya katika kufunga mabao baada ya kuifikia rekodi ya mkongwe Sir Bobby Charlton ya magoli 249 katika orodha ya wafungaji bora wa Manchester United.
- Kama Liverpool itashinda leo itaweka rekodi ya kufikisha pointi 47 baada ya michezo 21 katika ligi kuipita ile ya pointi 46 msimu wa 2008-09.
- Liverpool wasiposhinda leo watakua wamefikia rekodi ya kucheza mechi 4 bila kushinda katika mashindano yote mwanzo wa mwaka tangu mwaka 1993..

No comments