BAADHI YA MAMBO NILIYOYAONA KWENYE MECHI YA MAN UNITED vs LIVERPOOL.



Kuna vitu waweza ukashangaa ukiambiwa, lakini siku zote uhalisia wa jambo huja kwa mshangao.

Liverpool kujilinda kwa asilimia kubwa kwa mechi ya jana inaweza ikawa mshangao kwako, lakini ndiyo uhalisia wenyewe.

Walifaulu kwa kiasi kikubwa kuwa na nidhamu ya kujilinda pamoja na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kila walipokuwa wanashambulia walionekana wakali sana, kila walipokuwa wanashambuliwa walikuwa na upole na utulivu ambao kwa kiasi kikubwa uliwatala.

Mignolet anaweza akawa ameshaamka kutoka usingizini baada ya kushambuliwa sana na mashabiki na ikafikia hatua akawekwa benchi.

Jana alicheza vizuri sana, kitu pekee ambacho mabeki wa kati wa Liverpool wanakosa na kitazidi kuwagharimu ni,moja uwezo wao mdogo wa kucheza mipira ya juu pia kukosekana kiranja kati ya Klavan na Lovren, kuna wakati walikuwa hawajipangi vizuri hata zilipokuwa zinapigwa penetration passes ilikuwa ngumu kwao kuziblock.

Jana Manchester United walikuwa katika kiwango kizuri sana. Mabadiliko waliyoyafanya yalikuwa na manufaa makubwa sana.

Kutoka kwa Carrick na kuingia kwa Rooney huku kulikuwa na maana kubwa sana kwenye upande wa ulinzi pamoja na ushambuliaji kwenye timu ya United.

Kwa sababu, Pogba alitakiwa kurudi katikati na kucheza kama box to box midfielder. Kwenye timu unapokuwa na box to box midfielder unakuwa na faida zifuatazo, kwanza atahusika sana kwenye eneo la ukabaji, pili atahusika sana kwenye eneo la ushambuliaji kwa maana ya kwamba atakuwa anapandisha mashambulizi.Hivyo anatoa huduma mbili kwenye timu kwa wakati mmoja.

Pia Rooney alipoingia aliongeza uhai kwenye eneo la kushambulia akisaidizana na Zlatan.

Mabadiliko ya kuingia kwa Mata na Fellain kuchukua nafasi za Martial na Darmian kulikuwa na faida sana kwenye maeneo yafuatayo.

 Kwanza Mourinho alijua kabisa mabeki wa Liverpool siyo wazuri kwenye mipira ya juu. Hivyo kumwingiza Fellain kulikuwa na maana ya Fellain acheze eneo la mbele pamoja na Zlatan ambao wote ni warefu na wanaweza kucheza mipira ya juu kuliko mabeki wa Liverpool.

Na hii ilionesha matunda yake kwa sababu kabla ya goli kufungwa, Fellain alicheza mpira wa juu na ukagonga mwamba kabla haujamfikia Zlatan ambaye alikuwa eneo huru sana na kupiga mpira kwa kichwa na kufunga goli.

Kumchezesha Henrink katika eneo la beki wa kushoto lilikuwa na faida kubwa sana katika eneo la ushambuliaji maana kwa kiasi kikubwa alikuwa anapandisha mashambulizi kwa upande wa kushoto.

Anorld kiumri ni mdogo, ana miaka 18 lakini kwa kiasi kikubwa jana alifanya kazi nzuri.

Kwa umri wa miaka 18 kucheza kwenye mechi kubwa kama ile yenye presha ya hali ya juu na kucheza katika kiwango kikubwa ni kitu cha kumpongeza.

Sawa kuna wakati alionekana kuzidiwa katika maeneo fulani kama ya nguvu za kimwili ila kwa kiasi kikubwa alitimiza jukumu lake mama la kujilinda na kumfanya Martial asionekane na madhara makubwa sana.

Pia uwezo wake wa kupanda kushambulia huwezi ulinganisha na uwezo wa Nathan lakini kikubwa alichonifurahisha ni namna alivyokuwa anapamba na kuwahi kurudi kushambulia.

Kuingia kwa Countinho aliingia wakati ambao Man United ikiwa inatafuta goli kwa hiyo asilimia kubwa ya mipira ilikuwa inamilikiwa na United.

Lengo kubwa la Klopp ni kuongeza uhai wa mashambulizi ya kushtukiza na hili alifanikiwa kwa sababu pindi Countinho alipokuwa anapata mpira alikuwa hatari sana.

Ile khali ya kuwa na nguvu ya Upiganaji, kupambana mpaka mwisho ili wapate points ndicho kitu pekee kinachotofautisha kikosi cha Mourinho na vikosi vya Daudi Moyes na LVG.

Martin Kiyumbi

No comments

Powered by Blogger.