SERIE A: JUVENTUS YALIZWA NA FIORENTINA,LAZIO NA NAPOLI WAPETA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Italia Juventus jana ilipoteza mchezo wa nne msimu huu ikikubali kichapo cha bao 2-1 ugenini dhidi ya Fiorentina.
Juventus ambao bado wanaongoza msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa licha ya kufungwa jana walitangulia kufungwa bao la kwanza Nikola Kalinic akifunga bao hilo ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Milan Badelj alifunga bao la pili kwa Fiorentina kabla ya Gonzalo Higuain hajaifungia Juventus bao la kufutia machozi na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Ushindi wa bao 2-1 kwa wenyeji Fiorentina.
Katika mechi zingine hiyo jana Napoli walishinda kwa bao 3-1 wakiifunga Pescara huku AS Roma wakiifunga Udinese bao 1-0 na Lazio wakiilaza Atalanta bao 2-1. Sassuolo waliinyuka Palermo bao 4-1 huku Cagliari wakiifunga Genoa 4-1 pia.
Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha Juventus wanaongoza wakiwa na pointi 45 wskifatiwa na Roma wenye pointi 44 huku Napoli akishika nafasi ya tatu na pointi 41.

No comments