MAN UNITED,MAN CITY KICHEKO HUKU LIVERPOOL IKITOKA SARE NA "VIBONDE"

Ligi kuu ya England ilianza mzunguko wake wa pili jana kwa mechi 6 kupigwa katika viwanja 6 tofauti nchini humo.

Furaha ilikua kwa vilabu vya Manchester Yani Manchester United ikiwa ugenini ikishinda bao 2-0 dhidi ya West Ham huku Manchester City wao wakiibuka na ushindi wa bao 2-1 nyumbani dhidi ya Burnley.

Matokeo hayakua mazuri kwa Liverpool kwani ilikosa nafasi ya kuikaribia Chelsea katika msimamo wa ligi hiyo ikikubali sare ya bao 2-2 na Wenyeji Sunderland katika dimba la Mwangaza.

Daniel Sturadge na Sadio Mane walifunga mabao ya Liverpool lakini Penati mbili zilizofungwa na Jermaine Defoe ziliiharibia Liverpool kupata pointi zote tatu jana.

West Brom wao waliendeleza matokeo mazuri wakishinda 3-1 dhidi ya Hull City wakati mabingwa Leicester City wakibanwa mbavu na  Middlesbrough wakati Everton ikaizamisha Southampton bao 3-0.

Ligi hiyo itaendelea tena leo na hii ndiyo ratiba kwa muda wa Hapa nyumbani

●  Bournemouth vs Arsenal {saa 4:45 usiku}
●  Crystal Palace vs Swansea {Saa 5 Usiku}
●  Stoke City vs Watford {Saa 5 Usiku}

No comments

Powered by Blogger.