EVERTON WAKUTANA NA KIKWAZO KUMSAJILI MORGAN SCHNEIDERLIN WA MAN UNITED


Kiasi cha paundi milioni 19 kilichotengwa na Everton kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United Morgan Schneidelin kimekataliwa na uongozi wa Man United.

Habari kutoka katika vyanzo mbalimbali vya soka zimeeleza kwamba United wamewambia Everton kuongeza kiasi cha pesa kufikia paundi milioni 24 ambazo walizotumia kumnunua Morgan toka Southampton mwaka 2015.

Morgan Schneiderlin amekua hapati namba katika kikosi cha United na amedhamiria kuondoka ili kuboresha kiwango chake katika dirisha hili la usajili

No comments

Powered by Blogger.