YANGA YAPIGA 6 KOMBE LA MAPINDUZI


Mabingwa wa Tanzania bara Yanga jana ilianza vyema michuano ya kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa bao 6-0.

Yanga ilitoa kipigo hicho katika mechi ya pili ya kundi B dhidi ya Jamhuri ya Pemba mchezo uliopigwa katika dimba la Aman Mjini Zanzibar.

Mpaka mapumziko tayari Yanga ilishafunga bao 4 magoli ya Simon Msuva aliyefunga magoli mawili sawa na Donald Ngoma huku Thaban Kamusoko na Juma Mahadhi wakifunga bao moja kila mmoja kipindi cha pili.

Mechi hiyo ya kundi B ilitanguliwa na mechi ya awali jioni ya jana kati ya Wenyeji Zimamoto ya Zanzibar na Azam FC toka Tanzania bara ambapo Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

No comments

Powered by Blogger.