LA LIGA JANA : REAL MADRID YARUDISHA HESHIMA,MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI ZA JANA LA LIGA HAYA HAPA

Baada ya kufungwa mechi mbili moja katika ligi na nyingine katika Copa Del Rey,Vinara wa ligi kuu ya Spain Real Madrid jana walirudi katika mstari wakiibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Malaga katika dimba la Santiago Bernabeu.

Katika hali ambayo haikuzoeleka mfungaji wa magoli yote hiyo jana alikua beki wa timu hiyo na nahodha Sergio Ramos huku goli pekee la Malaga likifungwa na Juanpi.

Valencia wakiwa ugenini walizinduka na kuilaza Villareal bao 2-0 magoli ya Carlos Soler na Santi Mina.

 Espanyol ikiwa nyumbani iliwalaza Granada bao 3-1 magoli ya Reyes,Pablo Piatti na Marc Navarro wakati bao pekee la Granada likifungwa na kiungo wa Manchester United anayecheza kwa mkopo katika klabu hiyo Andreas Perreira.

Alaves wakiwa nyumbani waligawana pointi na Leganes kwa kufungana bao 2-2 katika mechi nyingine hiyo jana.

Magoli ya Alaves yalifungwa na Victor Laguardia na Edgar Antonio Mendez huku Leganes ikifunga magoli yake kupitia kwa Guerrero na Pablo Insua.

Mechi kadhaa za ligi hiyo zitachezwa leo na ratiba utaipata hapa katika website yetu.

2 comments:

  1. Thanks for your insight for your fantastic posting. I’m exhilarated I have taken the time to see this. It is not enough; I will visit your site every day. BanThang TV

    ReplyDelete

Powered by Blogger.