AFCON 2017 : UGANDA YATUPWA NJE BAADA YA KUPOTEZA DHIDI YA MISRI
Wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika mashariki Katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2017 Uganda wametupwa nje baada ya kufungwa bao 1-0 na Misri.
Mchezo huo wa kundi D ulikua ni wa mwisho hiyo jana ukitanguliwa na mchezo baina ya Mali na Ghana ambao ulimalizika kwa Mali kufungwa bao 1-0 goli pekee la Nahodha wa Ghana Asamoah Gyan.
Mchezo wa Uganda ambao walionekana kuwakabili vyema Misri ambao waliweza kupata bao pekee dakika ya 89 ya mchezo huo likifungwa na Abdala El Said akiunganisha pasi ya Mohamed Salah.
Ghana ambayo imefikisha pointi 6 baada ya ushindi wa jana inatinga hatua ya robo fainali wakati Uganda ambao hawajapata pointi yoyote wanasubiri kukamilisha ratiba katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mali huku Misri wakiombea Uganda washinde mechi hiyo ili wapate nafasi ya kufuzu.
RATIBA YA LEO
● Cameroon vs Gabon
● Guinea Bissau vs Bukina Faso
Mechi zote zitaanza saa 4 kamili usiku

No comments