WACHEZAJI 7 CAMEROON WAGOMA KUZIACHA KLABU ZAO ULAYA KWAAJILI YA AFCON
Afrika na maajabu yake ndivyo unavyoweza kusema baada ya mlinzi wa Liverpool Joel Matip ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Cameroon kukamilisha orodha ya wachezaji 7 wa taifa hilo waliokataa wito wa kwenda kuitumikia nchi ya katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2017.
Matip mchezaji aliyejiunga na Liverpool msimu huu ametaja sababu za kutotaka kujumuishwa katika kikosi cha timu hiyo ambayohajaichezea tangu mwaka 2014,kuwa ni maelewano mabayo kati yake na kocha aliyepita.
Mapema wiki iliyopita pia mchezaji wa beki ya kulia wa West Brom Allan Nyom nae alisema hataenda Gabon kwaajili ya michuano hiyo mikubwa kwa nchi barani Afrika huyu akitaja sababu kwamba anataka kuendelea kuaminiwa na kocha wake katika klabu ya West Brom baada ya kucheza michezo 14 msimu huu na hii imekua ndiyo sababu ya wengi kugomea timu za taifa.
Wachezaji wengine watano wa Cameroon ambao wamekataa kujiunga na timu hiyo na klabu zao kwenye mabano ni
- Andre Onana (Ajax Amsterdam),
- Guy N'dy Assembe (Nancy),
- Maxime Poundje (Girondins Bordeaux),
- Andre-Frank Zambo Anguissa (Olympique Marseille)
- Ibrahim Amadou (Lille).
Tayari orodha ya wachezaji 35 wametajwa na Cameroon kuelekea katika michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza januari 14.
Shirikisho la soka duniani FIFA katika sheria zake zinasema mchezaji atakayekataa kuitikia muito wa kulichezea taifa lake taifa hilo linaweza kuomba FIFA ikamfungiwa mchezaji husika kutocheza soka mpaka mashindano yatakapomalizika.
No comments