HATIMAYE FARID MUSSA KUPAA KESHO
Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania Farid Mussa anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Hispania kucheza soka la kulipwa.
Mussa anakwenda kujiunga na klabu ya Derpotivo Tennerife ya Hispania ambako aliripotiwa kufuzu majaribio tangu April mwaka huu lakini alikwama kujiunga na klabu hiyo.
Taarifa zinasema Farid alikwama kujiunga na timu hiyo kutokana na kuwa na matatizo wakati wa kuomba vibali vya kufanyia kazi nchini Hispania.
No comments