BOB BRADLEY ATUMBULIWA SWANSEA

Swansea City wametangaza kuachana na kocha wao mmarekani Bob Bradley ambaye waliingia nae kandarasi ya kukinoa kikosi chao mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.

Wamiliki wa klabu hiyo Steve Kaplan na Jason Levien wameamua kumtimua Bradley akiwa amekiongoza kikosi katika michezo 11 tu.

Pengine matokeo mabaya ndiyo chanzo cha Bradley kufungiwa virago haswa kipigo cha 4-1 walichokipata nyumbani kutoka kwa West Ham jana Desember 26.

No comments

Powered by Blogger.