BAADA YA USHINDI WA JUZI CHELSEA YAIFIKIA REKODI YA MAN UNITED, ARSENAL BADO VINARA WAO



Mbio za ubingwa kwa klabu ya Chelsea zimeendelea kutia matumaini baada ya juzi kushinda mchezo wake wa 12 mfululizo katika mwendelezo wa ligi kuu ya England.

Ushindi mara 12 mfululizo katika ligi unaifanya klabu hiyo ya London kufikia rekodi ya Manchester United kwa kucheza michezo 12 bila kufungwa wala kutoka sare kwenye ligi hiyo Man United ilifanya hivyo mwaka 2000.

Chelsea imebakiza mechi 2 tu kuifikia rekodi ya kucheza mechi 14 bila kufungwa inayoshikiliwa na Arsenal ambao walifanya hivyo mwaka 2002.

Ukiacha rekodi hiyo lakini zipo rekodi nyingine kadhaa ambazo Chelsea kwa kushinda mchezo wake dhidi ya Bournemouth wameweza kuziweka.

www.wapendasoka.com tumekuwekea rekodi hizo kama ifuatavyo:-

● Antonio Conte  anakuwa kocha wa kwanza kushinda mechi 15 za awali kati ya mechi zake 18 za ligi.

● Eden Hazard baada ya kufunga bao moja juzi amekua mchezaji wa 6 katika historia ya ligi kuu ya England kufunga magoli 50 kwa klabu ya Chelsea baada ya  Frank Lampard, Didier Drogba, Jimmy Floyd Hasselbaink, Gianfranco Zola na Eidur Gudjohnsen.

● Ni Hasselbaink (84), Drogba (106) na Gudjohnsen (153) pekee ndiyo wanaomzidi Hazard kwa kufikisha magoli 50 katika ligi kuu wakiwa wamecheza michezo michache kuliko Hazard ambaye juzi alicheza mchezo wake wa juzi

● Cesc Fabregas juzi alitoa assist yake ya 98 katika ligi kuu ya England anazidiwa na Wayne Rooney (101), Frank Lampard (102) Ryan Giggs (162) pekee katika historia ya ligi  hiyo.

1 comment:

Powered by Blogger.