YANGA KUJIULIZA KWA NDANDA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga leo watakua katika uwanja wa Uhuru kuwaalika Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Yanga itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza pointi 2 katika mchezo uliopita ambao walipata sare ya bao 1-1 na African Lyon.
Ndanda wao wameanza vibaya mzunguko wa pili wakipoteza mechi zote mbili mpaka sasa lakini wanajivunia sare ya bila kufungana katika mchezo wa awali dhidi ya Yanga kule Mtwara kwenye mzunguko wa kwanza.
Katika mchezo mwingine leo Mtibwa Sugar itaialika Maji Maji ya Songea katika viwanja vya Manungu Complex mkoani Morogoro.
Simba ndiyo Vinara wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwa wamejikusanyia pointi 41 wakifatiwa na Yanga wenye pointi 37 huku Toto Africans ikishika mkia pamoja na JKT Ruvu zote zikiwa na pointi 13.
No comments