LIVERPOOL YAENDELEA KUITISHA CHELSEA KILELENI EPL
Ikiwa nyumbani jana Liverpool iliweza kuifunga Stoke City bao 4-1 katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini England.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Anfield ulishuhudia Liverpool ikitangulia kufungwa kwa bao la Jonathan Walters dakika ya 12 tu ya mchezo lakini Adam Lallana aliisawazishia Liverpool dakika ya 35 ya mchezo kabla ya Roberto Firminho hajafunga bao la pili na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Liverpool wakiwa mbele kwa bao 2-1.
Kipindi cha pili Liverpool waliongeza mabao mengine mawili yakifungwa na Daniel Sturadge na goli la kujifunga la kiungo wa Stoke Imbula.
Kwa matokeo hayo Liverpool inafikisha pointi 40 katika nafasi ya pili pointi 6 nyuma ya Chelsea wanaoongoza ligi hiyo.

No comments