KILEVI CHAMPELEKA FIRMINHO WA LIVERPOOL MAHAKAMANI


Mwezi mmoja tangu Yaya Toure apigwe Faini ya paundi 54,000 na kuzuiwa kuendesha gari kwa mwaka mmoja na nusu alipokamatwa akiendesha gari huku amelewa, mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firminho naye amekumbwa na balaa hilo.


Firminho alikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Christmas akiwa amelewa huku akiendesha gari mitaa ya Merseyside na kukamatwa na polisi wa mji huo.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25 atatakiwa kusimama mahakamani kujitetea tarehe 31 Januari 2017 siku ambayo Liverpool watakua na kibarua kigumu kucheza mchezo wa ligi dhidi ya vinara Chelsea.

No comments

Powered by Blogger.