MIROSLAV KLOSE ATUNDIKA DALUGA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 38
Na Richard Leonce
Mshambuliaji mahiri Mjerumani Miroslav Klose ametangaza rasmi kuachana na soka leo akiwa na umri wa miaka 38.
Klose ambaye alistaafu soka la kimataifa baada ya kuiongoza Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 amekua bila klabu baada ya kuachana na Lazio katika majira ya joto mwaka huu.
Klose amewahi kuzichezea pia FC Homberg, FC Kaiserslautern, Werder Bremen na Bayern Munich, huku akiwa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Ujerumani akifunga mabao 71 katika michezo 137.
Rekodi za Klose haziishii hapo kwa sababu ndiye mfungaji bora wa fainali za kombe la dunia akiwa na jumla ya mabao 16 akiyafunga katika fainali 4 alizoshiriki.
Shirikisho la soka nchini Ujerumani DFB limethibitisha kupokea taarifa ya kustaafu kwa Klose, na limesema atajiunga moja kwa moja na benchi la ufundi la timu ya taifa hilo kama sehemu ya mafunzo ya kumwandaa kuwa kocha siku za usoni
No comments