VIJANA 12 MOROGORO WAULA AZAM FC

..Klabu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam juzi Jumapili Iliendesha kliniki ya kusaka vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.




Jumla ya vijana 528 walijitokeza katika kliniki hiyo ya aina yake inayosimamiwa na mtaalamu wa soka la vijana wa klabu hiyo inayoamini katika kukuza na kuendeleza vijana nchini raia wa Uingereza Tom Legg.

Vijana 32 waliweza kufika hatua ya fainali na katika hao ni 12 tu waliopata nafasi ya kuchaguliwa na watajiunga sasa na shule ya soka ya Azam FC.

Morogoro ni mkoa wa  tatu kufanyika kwa kliniki hiyo baada ya mazoezi mengine mawili kama hayo kufanyika katika majiji ya Dar es salaam na Tanga ambapo jumla ya vijana 37 wameshachaguliwa katika vijana 2,073 waliojitokeza katika mikoa hiyo mitatu.

Zoezi kama hilo litaendelea tena Jumapili wiki hii kwa vijana wa Pemba na Unguja na litafanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar kuanzia saa 1 asubuhi.

Vijana waliozaliwa mwaka 2000,2001 na 2002 ndiyo walengwa wa kliniki hii wanatakiwa kufika na vyeti vyao vya kuzaliwa

No comments

Powered by Blogger.