NIKIPEWA MKATABA MPYA NITASAINI, ASEMA MERTESACKER
Nahodha wa Arsenal mjerumani Per Mertesacker amefunguka leo kwamba kipao mbele chake kwa sasa ni kusalia katika kikosi cha washika bunduki hao wa jiji la London.
Per yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu huku akiwa katika wakati mgumu wa kukosa nusu nzima ya msimu huu kwa jeraha la goti.
Maisha ya Mertesacker ambaye amekua akihusishwa na mipango ya kurejea Ujerumani ambako klabu za Hannover na Werder Bremen zinatajwa kumwania yanaweza kuwa kwenye wasiwasi kutokana na kutoeleweka kwa uwepo wa kocha Arsene Wenger msimu ujao. Wenger pia yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
Arsene Wenger amekua na kawaida ya kutotoa mikataba ya zaidi ya mwaka mmoja kwa wachezaji wenye zaidi ya umri wa miaka 30, hivyo iwapo Mertesacker atapewa mkataba mpya atapaswa kulitarajia hilo kutokana na umri wake wa miaka 32.
Arsenal imekua ikifanya vizuri mpaka sasa msimu huu bila ya nahodha wake huyo ikishika nafasi ya pili katika ligi kuu huku ikiongoza kundi lake katika ligi ya mabingwa barani ulaya.
Atakaporejea Mertesacker huenda akakutana na upinzani mkali wa namba kutokana na beki mpya Shkordan Mustafi kuonekana kuelewana vema na Laurent Koscielny katika safu ya ulinzi.
"Mkataba mpya na Arsenal ndiyo kipao mbele kwangu japo bado hatujapanga tarehe ya mazungumzo. Mengine yote mnayoyasikia ni tetesi tu"
Na Richard Leonce

No comments