BASTIAN BADO ANA NDOTO ZA KUICHEZEA TENA MAN UTD.


Na Richard Leonce

Duru zinasema kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Chicago Fire ya ligi kuu ya Marekani na huenda akajiunga nao katika dirisha dogo la usajili wa majira ya baridi mwezi Januari.

Pamoja na hilo, Bastian amesema anaendelea kujifua  na yupo tayari kuichezea Man UTD tena iwapo atapata nafasi.

Itakumbukwa Bastian Schweinsteiger alirejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Man UTD hivi karibuni baada ya hapo awali kutakiwa na kocha Jose Mourinho kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa akiba.

"Ninaendelea kujiweka fit katika hali hii hii niliyopo, nina matumain ya kupata nafasi katika kikosi. Ninatazama mbele katika mazoezi na wenzangu kila siku."

"Sina hakika kama nitapata nafasi, lakini bado nipo vizuri katika umri huu wa miaka 32 na nina imani nitaendelea kucheza kwa miaka kadhaa mbele kwa kiwango cha juu na kushinda vikombe"

"Msimu uliopita tulishinda kombe la FA na hiyo ilikua moja kati ya ndoto zangu."

No comments

Powered by Blogger.