CHELSEA YAPANGA KUMREJESHA KUNDINI FRANK LAMPARD.

Klabu ya Chelsea imepanga kumrudisha kundini kiungo wake wa zamani Frank Lampard ambaye ana miaka 38 hivi sasa.

Lampard ambaye aliichezea Chelsea kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia New York City FC ya Marekani amemaliza mkataba wake wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo inayoshiriki MLS.

Lampard ni mmoja wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao Akiwa na New York City FC Lampard aliweza kufunga goli 15 katika mechi 31 wakati akiwa na Chelsea ameweza kuweznarekodi ya kuwa mfungaji bora wa klabu akifunga mabao 211.

Chelsea wanaogopa Yaliyowakuta Arsenal kwa mchezaji wao mwenye heshima klabuni kujiunga na mahasimu wao kama ilivyokua kwa Patrick Vierra ambaye alichukuliwa na Manchester City na hivi sasa anainoa klabu ya New York City FC.

No comments

Powered by Blogger.