MZAMIRU NDIYE MCHEZAJI BORA WA SIMBA OKTOBA
Kiungo wa Taifa Stars na Simba Mzamiru Yasin ameibuka kama mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo ambayo ni vinara wa ligi kuu Tanzania bara.
Wekundu wa Msimbazi Simba wamekua na utaratibu wa kuwazawadia wachezaji waliofanya vyema katika kila mwezi na kwa Mwezi Oktoba kura ya ushindi ilimwangukia Mzamiru Kiungo aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Katika kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwezi Oktoba Mzamiru amewashinda Shiza Kichuya na Mohamed Ibrahim wachezaji ambao wote watatu walicheza pamoja msimu uliopita katika klabu ya Mtibwa.
Mzamiru anakua mchezaji wa tatu kushinda tuzo hiyo ambayo huambatana na kitita cha fedha taslimu shilingi laki 5 za Kitsnzania. Wachezaji wengine ni Mohamed Hussein Zimbwe "Tshabalala" aliyeshinda mwezi Agosti na Shiza Kichuya aliyeshinda mwezi Septemba.
No comments