SPURS HAITAKI UJINGA YAWA TIMU YA KWANZA KUIFUNGA MAN CITY YA GUADIOLA

Tottenham Hotspurs imeingia katika rekodi mpya msimu huu baada ya kiwa timu ya kwanza kuifunga Manchester City inayofundishwa na Pep Guadiola ikiibuka na ushindi wa bao 2-0.



Mchezo huo uliopigwa katika dimba la White Hart Laine ni wa kwanza kwa Man City kufungwa katika michuano yote msimu huu huku Tottenham wakibaki kuwa timu pekee ambayo haijafungwa msimu huu katika ligi kuu ya England.

Kolorov alijifunga wakati akiokoa mpira wa krosi ya Danny Rose na kuipatia Spurs bao la kwanza kabla ya Delle Alli hajafunga bao la pili huku Eric Lamella akikosa penati

Kwa matokeo hayo Spurs inapanda mpaka nafasi ya pili ikifikisha pointi 17 pointi moja nyuma ya Man City wanaoongoza.

No comments

Powered by Blogger.