BAO LA DAKIKA YA MWISHO LAFUTA NDOTO ZA SERENGETI BOYS KUFUZU

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys imeshindwa kufuzu kucheza fainali za vijana Barani Afrika kwa kutupwa nje na Congo Brazaville.



www.wapendasoka.com imepata matokeo halisi toka uwanjani yanayothibitisha kwamba Serengeti Boys imeshindwa kufuzu baada ya kukubali kufungwa goli pekee katika mchezo wa leo dhidi ya Wenyeji ikiwa ni goli la dakika ya 92 wakati wengi wetu tukiamini kwamba vijana hao wamefuzu kama mchezo ungemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Matokeo ya bao 3-2 ambayo Serengeti iliyapata wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam ndiyo yamewaangusha leo kwani Congo Brazaville wamenufaika na faida ya goli la ugenini huku Serengeti boys ikishindwa kufunga bao lolote ugenini.

Mioyo ya Watanzania Wapenda Soka waliweka matumaini makubwa kwa timu hii kutokana na kiwango bora na maandalizi ya uhakika.


No comments

Powered by Blogger.