MWAMBUSI KUWACHEZESHA JKT RUVU MUZIKI WA PLUIJM ULIOWATESA KAGERA SUGAR.
Unaweza kuiita 'Pluijmless Yanga' leo ikiwa bila ya kocha wao kipenzi Hans Van Pluijm ambaye alijiuzulu siku mbili zilizopita.
Yanga wanaingia uwanja wa Uhuru leo kuwakabili JKT Ruvu katika mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu ya Vodacom wakiongozwa na kocha msaidizi Juma Mwambusi.
Tayari Mwambusi ametangaza kikosi kitakachowavaa maafande hao kutoka Mlandizi Pwani kikiwa na mabadiliko kidogo sana kutoka kile kilichoibuka na ushindi mnono wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mwishoni mwa juma lililopita.
Katika safu ya ulinzi, Yanga wataanza na Vicent Bossou badala ya Andrew Vicent ambaye ataanzia benchi.
1. Benno Kakolanya
2. Mbuyu Twite
3. Oscar Joshua
4. Andrew Vicent
5. Amisi Tambwe
6. Juma Mahadhi
7. Geofrey Mwashuiya
No comments