BMT WAWEKA NGUMU MABADILIKO YA UENDESHAJI WA SIMBA NA YANGA.
Katibu mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amezungumza na wanahabari leo juuvya msimamo wa baraza hilo kuhusu mchakato wa mabadiliko katika vilabu vya Simba na Yanga ambao upo katika vuguvugu la aina yake.
Kiganja amesema kuwa vilabu hivyo vinapaswa kurekebisha katiba zao kwanza kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9) .
Kiganja amesema kuwa mabadiliko yanayoendelea kwenye vilabu hivyo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kupinga michakato hiyo kitu ambacho sio kizuri na pia sio ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.
"Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa Wanachama kwenda kwa wawekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapo fanya mabadiliko kwa mujibu wa Katiba za Klabu zao," alisema Kiganja.
Aidha BMT imemtaka mdau au mwanachama yoyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye vilabu hivyo ni vema angeanzisha timu yake kama Saidi Salum Bakhresa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko kwavile timu hizo zina Wanachama wengi.
Kiganja amesema kuwa michakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote kwani mabadiliko yoyote ndani ya klabu hizo lazima yafuate Katiba zao.

No comments