MAISHA YANAENDELEA: YANGA KULA KIPORO BILA PLUIJM LEO

Mabingwa watetezi wa ligo kuu Tanzania bara Yanga itaingia dimbani leo kumenyana na maafande wa JKT Ruvu katika mechi ya kiporo ya ligi hiyo.


Mechi ya leo itakayopigwa katika dimba la Uhuru Uhuru itakua ya kwanza kwa Yanga kucheza bila ya kocha Hans van der Pluijm aliyetangaza kung'atuka kama mkuu wa ufundi wa klabu ya Yanga kufatia tetesi za kuletwa kocha mwingine kwenye nafasi yake.

Yanga itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 6-2 katika mechi iliyopita dhidi ya Kagera Sugar kule Bukoba wakati JKT Ruvu wao wakipoteza kwa bao 1-0 dhidi Azam FC.

Yanga inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kibwa zaidi katika ngazi ya klabu hapa Tanzania wakati JKT Ruvu wao wakikamata nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.