MOURINHO AU GUADIOLA LEO KUPOTEZA UBINGWA WA KWANZA MSIMU HUU KATIKA DIMBA LA OLD TRAFFORD
Mechi za mwisho za hatua ya Robo fainali ya michuano ya kombe la Ligi (EFL) Nchini England inaendelea leo kwa mechi 3 kupigwa katika viwanja vitatu.
Mechi kubwa ya leo na ni mechi kubwa katika michuano hiyo kwa miaka kadhaa ni kati ya Manchester United watakaokua nyumbani kiwaalika Manchester City katika dimba la Old Trafford.
Mechi hizi ni za mtoano na ni lazima mshindi apatikane hata kwa penati hivyo ni dhahiri timu mojawapo itapoteza nafasi ya kutwaa kombe hili msimu huu.
Baada ya kichapo kutoka kwa Chelsea Kocha Jose Mourinho yuko katika mtihani mwingine wa kupata matokeo mbele ya watazamaji zaidi ya 60,000 katika dimba la Old Trafford huku Pep Guadiola akitafuta ushindi wa kwanza baada ya mechi 5 bila kupata ushindi.
Timu hizo zilishakutana katika ligi kuu msimu huu Man City ikashinda kwa bao 2-1 Magoli ya Iheanacho na Kevin De Bryune huku Zlatan akifunga bao 1.
Man United itamkosa Eric Bailly aliyeumia katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea wakati De Bryune naye ni majeruhi kwa upande wa Man City.
Mechi zingine leo itakua baina ya Chelsea na West Ham wakati Sunderland watacheza dhidi ya Southampton.
Mechi zote hizi zitaanza saa nne kasorobo usiku isipokua mechi ya Manchester itakayoanza saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments