MSHAMBULIAJI SPURS NDIYE BORA KABISA EPL SEPTEMBA, AWEKA REKODI MPYA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Korea Kusini anayeichezea Tottenham Hotspur Son Heung-Min amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi katika ligi kuuvya England kwa mwezi wa tisa.



Son anakuwa mchezaji wa kwanza toka Bara la Asia kushinda tuzo hiyo inayotolewa kila mezi kwa mchezaji mmoja anayefanya vizuri zaidi katika mwezi husika.

Son mwenye miaka 24, alifunga magoli manne mwezi wa Tisa akiisaidia Tottenham kuendelea kutamba msimu huu wakicheza bila kupoteza mchezo wowote na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Mchezaji huyo ambaye bado kidogo tu auzwe kabla msimu haujaanza Alifunga mabao mawili dhidi ya Stoke City wakati Spurs ikishinda bao 4-1 kisha akafunga mabao mawili tena katika ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Middlesbrough.

Son amewashinda Adam Lallana wa Liverpool, Romelu Lukaku wa Everton,Kevin De Bruyne wa Manchester City na Theo Walcot.

No comments

Powered by Blogger.