NI WIKIENDI NYINGINE YA LIGI KUU BARA, ISRAEL NKONGO KUSIMAMA KATIKATI YA AZAM NA YANGA.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa michezo mitatu ambapo Simba inayoongoza msimamo itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Hussein Athuman kutoka Katavi ambapo pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa Kilimanjaro. Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.
Huko Mabatini Pwani nj JKT Ruvu dhidi ya Mwadui ya Shinyanga. ambao watachezeshwa na Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed wa Dar es Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.
Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani na Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.
Stand United ya Shinyanga itaikaribisha African Lyon huko CCM Kambarage, sheria 17 zikisimamiwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba akiwa Joseph Pombe wa Shinyanga. Kamishna atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.
Baada ya kesho Ligi hiyo itaendelea tena keshokutwa Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu za Azam na Young Africans za Dar es Salaam katika nyasi bandia za uwanja wa Uhuru.
Kipyenga kitaamrishwa na pumzi za Mwamuzi Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.
Ruvu Shooting wao watawaalika Mbeya City nyumbani Mabatini mkoani Pwani. Maamuzi ya mchezo huo yatakuwa chini ya Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam.
Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.
Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo utachezeshwa na Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba ni Nicolaus Makalanga wa Morogoro.
Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Toto African na Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Utachezeshwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.

No comments