MCHEZAJI HUYU ANAWINDWA ILI KUTIBU TATIZO LA BEKI MAN UNITED

Anaitwa ANTONIO RUDIGER
- Beki wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia akiwa na umri wa miaka 23 anacheza kama beki wa kati na hata beki wa kulia.



Taarifa zinasema Manchester United tayari wameanza mazungumzo ya kunasa saini ya beki huyu ili kusaidiana na Eric Bailly katika nafasi ya beki wa kati.

Inasemekana kocha Jose Mourinho hajafurahishwa na uwezo wa mabeki waliopo Kikosini yani Chriss Smalling,Marcos Rojo na Daley Blind na huenda huu ukawa msimu wao wa mwisho kuichezea Manchester United.

Taarifa zilizopo zinasema kiasi cha Paundi milioni 35 kimetengwa kuwashawishi Roma kumuuza mchezaji huyu anayewaniwa pia na Antonio Conte kocha wa Chelsea.

No comments

Powered by Blogger.