NGUVU YA MASHABIKI WA YANGA YAMREJESHA KOCHA PLUIJM KUNDINI
Siku ya tano tu baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu na ombi lake kukubaliwa na viongozi, Yanga wametikisa vichwa wakasema 'haiwezekani, mzee wetu rudi hapa'.
Taarifa tuliyoipata inasema tayari Yanga wamemwandikia Hans barua ya kukataa ombi lake la kujiuzulu, lakini pia wakimwomba aendelee kukifundisha kikosi cha wanajangwani hao.
Taarifa zinasema haikua rahisi kumshawishi Pluijm arejee Jangwani, na kama siyo ushawishi mkubwa kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani Mh Mwigulu Lameck Nchemba ambaye ni mwanachama na shabiki wa wazi wa klabu hiyo, pengine mambo yangekwama.
Pluijm ambaye alijiuzulu baada ya kushtukia kwamba Yanga wanafanya mazungumzo na kocha mwingine pasipo kumtaarifu, alihudhuria mchezo wa katikati ya juma ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu yeye akiwa jukwaani.
Baada ya mchezo huo wapendasoka.com ilishuhudia gari la kocha huyo likizuiwa na mashabiki wa Yanga kama njia ya kuonesha mapenzi yao kwa kocha huyo ambaye anakubalika sana kwa wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo.
Japo bado haijafahamika ni lini Pluijm atajiunga tena na kikosi cha Yanga, lakini kurejea kwake kunamaanisha kufa kwa mazungumzo ambayo Yanga walikua nayo na kocha Mzambia George Lwandamina.

No comments