KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : TATHMINI YA WAPENDA SOKA KUELEKEA KATIKA MECHI YA WATANI LEO

Pambano la watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga na Simba linapigwa alasiri ya leo jijini Dar es Salaam.

Kupitia KIJIWE CHA WAPENDA SOKA tumeweza kuongea na baadhi ya wadau kuona nini mtazamo wao kuelekea katika pambano hilo.



Richard Leonce Chardboy: 

Ni ngumu kuuchambua huu mchezo kwa sababu mara nyingi huwa hautawaliwi sana na mbinu sahihi za kiufundi, ni mara nyingi tunashuhudia aina ya soka tusiyoitarajia katika mtanange huu lakini bado haituzuii kuuchambua.

Baada ya muda mrefu nadhani Simba wana nafasi nzuri sana ya kushinda huu mchezo kama watatulia kwenye mfumo wao ambao wamekua wakiutumia tangu ligi ianze.

Yanga hawapo vizuri, wanaweza kuwa na wachezaji wazuri wenye vipaji na uzoefu zaidi ya Simba lakini wengi wamechoka, hawajapumzika tangu walipoanza msimu uliopita wa 2015/16.

Kwa Simba mpya, yenye muunganiko mzuri wa vijana wadogo, ina nafasi kubwa sana ya kuwasumbua Yanga jioni ya leo na hata kuibuka na ushindi.

Kitu pekee kinachoweza kuwagharimu Simba ni aina yao ya mchezo, wamekua wakipiga pasi fupi fupi nyingi bila kusogea mbele, na wanapoteza mipira kirahisi sana. Hili linaweza kuwadhuru kama wasipolifanyia kazi kwa sababu Yanga ni wazuri katika kupora mipira na kupiga pasi sahihi kwa wakati sahihi.

Jonas Mkude ndiye mchezaji Muhimu sana kwenye kikosi cha Simba leo. Huyu ndiye atakayeamua kama Simba itawalike au isitawalike katika eneo la kiungo ambalo bila shaka atakua akipambana na Thabani Kamusokho.

Kwa upande wa Yanga nadhani watatumia zaidi uzoefu wa Kamusokho na Mbuyu Twite katikati ya kiwanja na mchezo wao utakua ni ule ule wa pasi ndefu na wa kutumia mawinga wao.

Naitabiria Simba ushindi wa tofauti ya goli moja.

Bab Chico: 

Yanga anaingia akiwa na kumbu kumbu ya kumfunga mtani wake bao 2-0

Yanga hawajaanza vizuri Ligi safari hii hii haimaanishi kuwa atafungwa leo Mara nyingi mechi hii haihusiani na kiwango chako ni mechi ya watani wa jadi INA mambo mengi ndani yake

Kama Yanga watatumia vizuri nafasi watakazopata na kuweza kuzuiya Viungo wasimba wasitengeneza nafasi basi watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda

SIMBA wanaingia katika game hii wakijiamini sana na hili kwa mechi za watani Mara nyingi linakuwa tatizo

Simba wamefanya usajili mzuri kama wataweza kuwahimili Yanga kwenye kiungo chao basi simba w anaeza kupata matokeo ubora wa Beki ya Yanga unaeza kuwa kikwazo cha matokeo

Ushindi wa Simba unategemea Ajib atavoweza mtengenezea nafasi Mavugo

Yanga 1-1 Simba

Edo DC: 

Moja ya mitanange mikubwa ya watani wa jadi barani Afrika ni huu wa Yanga na Simba na leo kwa mara nyingine na ni mara ya kwanza katika ligi Kuu ya Soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2016/2017.

Pambano la leo katika uwanja wa Taifa linavikutanisha vilabu vikongwe hapa Tanzania vyenye wapenzi wengi zaidi huku Simba wakiongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo 6 huku Yanga wao wakiwa na pointi 10 baada ya michezo mitano katika nafasi ya 3.

Msimu uliopita Yanga iliinyanyasa Mno Simba kwa kushinda michezo yote miwili lakini msimu huu ni tofauti kidogo kwasababu ya uimara wa kikosi cha Simba tukitegemea kuona ushindani mkubwa tofauti na msimu uliopita.

Simba inajivunia kwa kuwa na safu nzuri sana ya kiungo ikiongozwa na nahodha Jonas Mkude ambaye mara nyingi hucheza kama kiungo mkabaji nategemea pia kocha Omog atamchezesha pia Said Ndemla au Mwinyi Kazimoto kwaajili ya kusaidia katika mashambulizi.

Leo itakua mashindano ya safu za ushambuliaji kwanza Simba ambao wana KIAMA chini ya Laudit Mavugo,Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib imeonekana kama ni safu bora kabisa kwa sasa ikiwa imeshafunga mabao 9 wakati Yanga wao wana MSN wakiwa na Donald Ngoma,Amiss Tambwe na Simon Msuva ambao wameshafunga mabao matano.

Kitovu cha soka la Tanzania kiko kwa timu hizi na ndicho watu wengi tunatarajia kuona leo kwani Simba ina wachezaji 7 na Yanga wachezaji watano katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania.

Natabiri Simba kushinda 2-1

FESTO NGALAWA (FES)


Mara nyingi mechi zao huwa tamu nje ya uwanja zaidiiii
tambo mbali mbali za watani wa jadi hunogesha pambano zaidiii

Mechi kubwa Tanzania hadi afrika mashariki
Timu hizi zina wapenzi wengi sana Tanzania na afrika mashariki.Na ndio timu kubwa na kongwe nchini.

Leo tarehe 1/10/2016 timu hizi zinakutana katika mzunguko wa kwanza wa ligi hii ya msimu wa mwaka 2016/2017.

Simba wanaingia katika pambano hili wakiwa wageni na yanga wakiwa Wenyeji wa mchezo
Yanga anafaida zaidi maana katika msimu uliopita alishinda mechi zote mbili za ligi kwa idadi ya mabao 2 kwa kila mechi
Kwa utaalamu wa mpira inawapa ujasiri zaidi kuwakabili simba.

Simba yenyewe inaingia katika pambano hilo ikiwa na ujasiri kwa sababu toka ligi ianze hawajafungwa mechi hata moja na ndio wanaongoza ligi na hata wafungwe bado wataongoza ligi tu.
Hicho katika utaalamu wa mechi kinampa ujasiriii kabisa wa kuwakabili yanga.

Mechi hii inamvuto wa Mengi
-ushindani wa wachezaji wa kigeni
Kwa upande wa yanga
NGOMA
KAMUSOKO
TAMBWE
CHIRWA

Simba nao wanaomajembe wao wa nje
MAVUGO
MWANJALI
BOKUNGU
AGBAN
BRAGNON

-Pacha ipo kali??
Yanga wamecheza muda mrefu wao wanaonekana kuzoeana zaidiii kuna pacha yao kali ambayo inaongozwa na
Ngoma
Msuva
Tambwe

Simba nao hali siyo mbaya wana pacha yao kali sana
Mavugo
Ajib
Kichuya

-wadhamini wa timu hizo
Kila timu inaonekana imejiandaa hadi kifedha
Yanga ikiwa na tajiri wao mhindi MANJII ambae anawadhamini yanga kupitia kampuni yake ya QUALITY
SIMBA nao msimu huu hawatishiki kwa suala la fedha maana Tajiri kijana Afrika MOHAMED DEWJI Ameamua kwa dhati kuidhamini simba.

-mashabiki
Ushawahi kuona mashabiki vichaa wa mpira wa Tanzania wanapatikana SIMBA NA YANGA
huwa wanaugonjwa wao wa kuzimia kwa kuambukizanaaa aiseeee
Kama maajabu vile utashangaa yanga wanazimia na simba wanazimiaaaa.
Tambo zao sasa ndio hatarii wanatambiana hadi kwenye UCHAWIII
Yaani FULL VIOJA mashabiki wa Simba na yanga.

-Makocha
Pia ni kivutio cha mechi
Kocha wa Yanga yuko vizuri sana na ndiye kocha anaeshikilia tuzo bora ya kocha bora wa msimu uliopita hivyo ubora wake unajulikana.
Pia yupo mwambusi kocha msaidizi yuko vizuri sana ukitaka kulijua hilo mkumbuke mbeya cty ule msimu wake wa kwanza ligi kuu.
Vipi kuhusu Kocha wa simba je unajua Azam wana taji moja la ligi kuu toka ianzishwe
Sasa kwa taarifa yako hilo taji walilipata kupitia OMOG ambae ni kocha wa simba kwa sasa hivyo ni kocha mzuri sana.
Pia yupo mayanja kocha msaidizi wa Simba ambae aliiongoza simba kwa msimu uliopita.
Naamini ufundi wa makocha nitauona ktk mechi ya leo.

KILA LA KHERI YANGA VS SIMBA NAWATAKIA MECHI NZURI NA TAMU

Utabiri wangu
Yeyote anapigwa
Ila mechi itaisha kwa sare

Kwa leo ni haya Tu tukutane siku nyingine.

No comments

Powered by Blogger.