HII HAPA HABARI KAMILI YA FARID MUSA KWENDA HISPANIA KUCHEZA SOKA

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifa wapenzi wa soka kuwa winga wao Farid Mussa, leo amepata kibali rasmi cha kufanya kazi nchini Hispania.


Kwa muda mrefu Azam FC imekuwa ikisubiria kibali hicho ili mchezaji huyo akaanze maisha mapya ya soka nchini humo katika timu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kufuatia kibali hicho kupatikana, Mussa anatarajia kuondoka nchini muda wowote kuanzia sasa kwenda kuitumikia timu hiyo.
Tunapenda mashabiki wa soka watambue kuwa Mussa anakwenda Tenerife kwa kwa makubaliano maalumu ya pande zote mbili ukiwa ni usajili wa mkopo na Azam FC itanufaika kupitia uhamisho wake mwingine atakaposajiliwa kwenda timu nyingine barani humo.
Tunaamini uwepo wake kwenye klabu hiyo utafanikisha kukuza kipaji chake zaidi pamoja na thamani yake kwa ujumla, ukizingatia bado ni mchezaji kijana anayeendelea kujifunza.
Kabla ya kibali hicho kutoka, kuna taarifa mbalimbali zilizotolewa zikiihusisha Azam FC kuwa tumemzuia kijana wetu huyo kujiunga na timu hiyo, lakini inaomba ieleweke kuwa kibali kilichotolewa leo hii ndicho kilichokuwa kikikwamisha uhamisho huo na tunamshukuru Mungu kimepatikana.
Tunaomba ieleweke kuwa, Azam FC haitafanya jitihada zozote za kuziba milango ya wachezaji wetu pindi watakapopata timu nje ya nchi, sisi tutakuwa wa kwanza kuwaongoza katika kufikia malengo yao makubwa ya kucheza soka la kulipwa kwenye maslahi mazuri endapo taratibu za usajili zitafuatwa.
Azam FC tunapenda kuishukuru Tenerife kwa kufanikisha uhamisho huo na tunamtakia mafanikio mema Mussa katika maisha yake mapya ya soka na tunaamini ataitangaza vilivyo timu yetu kimataifa na Tanzania kwa ujumla jambo ambalo litafungua milango kwa wachezaji wengine kuungana naye huko.
Imetolewa na Uongozi wa Azam FC
Kibali cha Farid 

No comments

Powered by Blogger.