YANGA HII SASA SIFA, ENEO LAO LA KUJENGA UWANJA KIGAMBONI NI MARA 26 YA LILE LA SIMBA BUNJU

Mabingwa wa Soka Tanzania bara Yanga jana walizindua ujenzi wa uwanja wao katika eneo la hekari 715 Kigamboni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua mojawapo katika kukamilisha ndoto ya muda mrefu ya kuweza kujenga uwanja wao.
Wasaidizi wa Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe kabisa Yusuph Manji wamekabidhi eneo hilo jana mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo na Maofisa wa Serikali ya wilaya mpya ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu hiyo ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Katika eneo hilo ambalo utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine pamebatizwa jina la kijiji cha Yanga SC.

Eneo hilo la Yanga ni mara 26 zaidi ya eneo la Simba la hekari 27 ambalo liko Bunju na kwa namna ya kipekee www.wapendasoka.com inapenda kupongeza juhudi za vilabu hivi viwili katika kufanikisha ndoto ya muda mrefu.

No comments

Powered by Blogger.