MAJIMAJI WAKUTANA NA KIAMA CHA SIMBA WAGARAGAZWA VIBAYA TAIFA.

Vinara wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wameendeleza ushindi katika mechi zao za ligi kuu baada ya kuinyuka Maji Maji ya Songea kwa bao 4-0.



Simba ambayo ilionyesha kiwango bora kabisa hasa kipindi cha pili wakimiliki mpira na kupiga mashuti mengi golini na mpaka mapumziko walishakua mbele kwa bao 1-0 goli pekee la Jamal Mnyate.

Kipindi cha Pili Simba iliongeza mashambulizi na kupata mabao mengine matatu yakifungwa na Shiza Kichuya magoli mawili na Jamal Mnayate aliyefunga tena goli moja na kumfanya kufunga magoli mawmoj katika mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kukalia uongozi wa ligi hiyo wakiwa na pointi 16 huku Majimaji wakibaki katika nafasi ya mwisho wakiwa hawana pointi yoyote.

No comments

Powered by Blogger.