ALICHOLISEMA MOURINHO BAADA YA KUMWEKA BENCHI ROONEY, UNITED ILIPOIFUNGA LEICESTER LEO

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa kumwacha Wayne Rooney katika bench wakati Timu hiyo ikiikandamiza Leicester City bao 4-1.


" Nikijua mngeniuliza swala hili la kwanini nimemwacha Wayne katika bench lakini nadhani ingekuwa sawa kama mngeniuliza kwanini nimewachezesha Lingard na Rashford" Alisema Mourinho.

"Rashford na Lingard walipaswa kuanza kwasababu wana kasi na mchezo huo ulipaswa watu wenye kasi ili kushindana na kasi ya Leicester na ukiangalia mshambuliaji wetu [Ibrahimovic] alitakiwa kutengenezewa nafasi" Alimaliza kusema Mourinho.

Manchester United iliibuka na ushindi huo muhimu baada ya kupata matokeo mabaya katika mechi mbili za ligi zilizopita magoli yaliyofungwa na Chriss Smalling,Juan Mata,Marcus Rashford na Paul Pogba.

No comments

Powered by Blogger.