AZAM WAKUMBANA NA KICHAPO MTWARA,MBEYA CITY HOI KWA JKT RUVU

Azam FC wameendeleza wimbi la matokeo mabaya baada ya leo kukubali tena kichapo cha bao 2-1 toka kwa Ndanda FC.

Azam FC ikisafiri mpaka Mtwara imejikuta ikipoteza mchezo wake wa wa pili mfululizo katika ligi kuu msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mechi iliyopita dhidi ya Simba.

Katika mechi nyingine leo JKT Ruvu iliweza kuibanjua Mbeya City kwa bao 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la mabatini mkoani Pwani.

Huko Mbeya wenyeji Prisons walilazimishwa sare ya bila kufungana na Mwadui FC toka Shinyanga wakati Mtibwa walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbao FC toka Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.