KILIMANJARO QUEENS YATWAA UBINGWA NA KUWEKA REKODI YA NAMNA YAKE

Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Queens imetwaa ubingwa wa soka Afrika Mashariki na kati Kwa wanawake (CECAFA WOMEN CHALLENGE)


Queen imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya wanawake ya Kenya kwa kuichapa bao 2-1 mchezo uliopigwa jioni hii huko Uganda.

Magoli ya Kilimanjaro Queens yaliwekwa kimiani na Mwanahamisi Omary na Stumai Abdallah.

Kilimanjaro Queens kwa kutwaa ubingwa huo imekua timu ya kwanza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ambayo mwaka huu ndiyo mara ya kwanza inafanyika.

HONGERA KILIMANJARO QUEENS

No comments

Powered by Blogger.