KILICHOTOKEA JANA KATIKA LIGI KUU NCHINI ENGLAND HIKI HAPA

Baada ya Chelsea kufungwa na Liverpool wakiwa darajani hapo Ijumaa Ligi kuu ya kandanda ya England iliendelea tena jana Jumamosi kwa michezo kadhaa kupigwa.


Vinara wa ligi hiyo Manchester City wakiwa nyumbani wameendeleza ubabe wao kwa kuichapa AFC Bournemouth kwa goli 4-0.

Ushindi huo ni mwendelezo wa mwanzo wao mzuri wakiwa wameshinda michezo yote mitano ya mwanzo ikijiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

West Bromwich Albion ikaifunga West Ham United kwa goli 4-2 ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwa goli 4 baada ya miaka 4.

West Ham ilifanya vyema sana msimu uliopita lakini mambo yameonekana kuwaendea kombo msimu huu. Ikiwa imeruhusu kufungwa goli 13 kwa msimu huu.

Baada ya sare ya bao 1-1 na PSG katika ligi ya mabingwa Ulaya Arsenal ikiwa ugenini imeifunga Hull City kwa goli 4-1 huku Sanchez akikosa penati. Ushindi huo ni wa 3 mfululizo kwa Arsenal.

Mabingwa Leicester City wakitoka katika ligi ya mabingwa barani Ulaya katikati ya wiki ambapo walishinda bao 3-0 huko Ubelgiji wameweza kutoa kipigo kama hicho kwa Burnley katika dimba la King Power.

Kwa Upande wao Everton walizidi kung'ara. Gareth Barry akicheza mchezo wa 600 katika ligi kuu alifunga goli moja. Ni Ryan Giggs na Frank Lampard pekee waliocheza michezo zaidi ya 600 wakaifunga Middlesbrough bao 3-1.

Ushindi ambao umeifanya klabu hiyo kuanza  vyema ligi baada ya miaka 38 kupita. Mara ya mwisho kuanza ligi vyema walimaliza wakiwa nafasi ya nne.

MATOKEO NA WAFUNGAJI

● Chelsea 1-2 Liverpool
Diego Costa (61')
                   Dejan Lovren (17')
                   Jordan Henderson (36')

● Hull City 1-4 Arsenal
Robert Snodgrass (79' PEN)
                      Alexis Sánchez (17', 83')
                      Theo Walcott (55')
                      Granit Xhaka (90'+2')

● Leicester City 3-0 Burnley
Islam Slimani (45'+1', 48')
Ben Mee (78' OG)

● Manchester City 4-0 AFC Bournemouth
Kevin De Bruyne (15')
Kelechi Iheanacho (25')
Raheem Sterling (48')
Ilkay Gündogan (66')

● West Bromwich Albion 4-2 West Ham United
Nacer Chadli (8' PEN, 56')
Salomón Rondón (37')
James McClean (44')
                   Michail Antonio (61')
                   Manuel Lanzini (65' PEN)

● Everton 3-1 Middlesbrough
Gareth Barry (24')
Seamus Coleman (42')
Romelu Lukaku (45'+1')
             Maarten Stekelenburg (21' OG)

LIGI HIYO ITAENDELEA TENA LEO JUMAPILI

••••Ligi ya uingereza itaendelea tena kesho jumapili 18/09/2016 kwa michezo minne.
Manchester United ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo yake miwili ya mwisho itamenyana na Watford katika mchezo utakaoanza mapema saa nane mchana.

2:00 PM - Watford vs Manchester United
4:15 PM - Crystal Palace vs Stoke City
4:15 PM - Southampton vs Swansea City
6:30 PM - Tottenham Hotspur vs Sunderland

~Abel Alvaro

No comments

Powered by Blogger.