NEEMA ZAENDELEA KUMWAGIKA KWA MOHAMMED HUSSEIN NDANI YA SIMBA
Wiki moja baada ya kupewa zawadi ya gari na mwenyekiti wa kamati ya Usajili katika klabu ya Simba bwana Zacharia Hans Pope, Mohamed Hussein Zimbwe aendelea kupata neema.
Mchezaji huyo ambaye anaimudu vyema nafasi ya ulinzi wa pembeni kushoto jana alipewa pia zawadi ya mchezaji bora wa mwezi Agosti ndani ya klabu hiyo.
Mohamed Hussein ambaye wengi hupenda kumwita Tshabalala alikabidhiwa jana zawadi hiyo pamoja na pesa taslimu shilingi laki 5 na Mtendaji mkuu wa EAG Group Imani Kajula kabla ya mechi na Azam FC katika uwanja wa Uhuru ambapo Simba ilishinda bao 1-0.

No comments