CHELSEA VS LIVERPOOL. GEGGENPRESSING VS HALF CATTENACCIO

Ni nadra sana kushuhudia kocha wa Kiitaliano kuwa na safu mbovu ya ulinzi. Hii ni sifa yao kutokana na makuzo yao ya kisoka. Kushangaa kwanini Fabregas anaweza kuachwa katika kikosi cha Conte ili Matic na Kante waanze kwa pamoja ni sawa na kujiuliza kwanini Coutinho ni mnyumbulifu, wakati unatambua ni Mbrazil. Waitaliano waliishi katika mfumo unaitwa Cattenaccio ambao uliwafanya kuwa na safu bora ya ulinzi na mfumo uliokera wengi kabla ya kupatiwa ufumbuzi na Total Football.


Leo Ijumaa wanakutana makocha wawili wenye falsafa tofauti kabisa. Klopp akiifundisha Liverpool anapendelea zaidi mfumo wa 433 huku akiwa hana mchezaji mgumu mgumu ili kuruhusu pressing kwa kiasi kikubwa katika eneo la mpinzani na kumzuia asije kwenye eneo lao. Mfumo huu unaibuka na falsafa inayoitwa Geggenpressing. Conte kwa upande wake atakuwa anajiuliza ni namna ipi akabe kwa umakini sana huku akimtumia Kante aliyepokonya mipira mara nyingi zaidi kwenye EPL msimu huu kujaribu kuwafanya Liverpool wasiishi kwa Amani huku akiwashambulia kwa kustukiza, udhaifu ambao uliwaua dhidi ya Burnley.

Ili Liverpool iwe imara kuipenya Chelsea na kuleta madhara inatakiwa kwa sasa Jordan Henderson apige pasi sawia sana na kuwafanya Wijnaldum pamoja na Lallana wacheze. Hii moja kwa moja itafanya Coutinho, Firmino, Mane pamoja na Sturridge kwa yeyote atakayekuwa kikosini waweze kuwa na hatari sana kwa maana ya mfumo wa 433 kuwa na madhara na hapa pressing yao inaweza kumwondoa mchezoni Ng'olo Kante.

Wachezaji wote wa Liverpool isipokuwa Sturridge wanajua kukabia kwenye eneo la adui, na wengi wanaweza wasijue kwanini Wijnaldum na Lallana ni wachezaji wa mbele lakini wanacheza katikati pembeni, hii ni ili kuifanya Liverpool kuwa na wachezaji wanaozunguka uwanja kwa umbali mrefu na kuwakata pumzi wapinzani.

Kwa Upande wa pili Liverpool wana safu mbovu ya Ulinzi huku wakikutana na Costa aliyekuwa kazaliwa upya na akiwa na msukumo wa kuendelea kufanya vyema. Klopp atatakiwa kuisuka vyema ngome yake huku akihakikisha Henderson aachi nafasi kubwa kati yake na eneo la ulinzi kwa tamaa ya kupenda sana kupress. Hivyo kuviziwa itakuwa kitu ambacho Conte atakuwa amepanga kukifanya na akipata nafasi atawaumiza na ni dhambi Chelsea kutangulia kupata goli kwa sababu kurejea kumbukumbu za mchezo wa Pre Season ni rahisi.

Ukuta wa Berlin ni kitu ambacho Conte atakifanya na ambacho anajua fika kuwa Liverpool ni dhaifu unapoketi nyuma kuwasubiri. Sema wakati huu haitokuwa kama Burnley kwa sababu kama timu kubwa atatakiwa kukaa na mpira pia. Magoli waliyoruhusu dhidi ya Swansea hawatakiwi kufanya vile dhidi ya Liverpool hii ambayo inaongoza kufunga mabao mengi mwaka huu tangu Januari.

Chelsea pia wanaweza kutumia mipira ya adhabu au kona kuwaadhibu Liverpool iwapo Mignolet ataanza kwa sababu hajui kuongoza eneo lake la ulinzi vyema. Kuna mchezaji anaitwa Victor Moses? Naam huyu atawafaa kama mchezaji wa akiba. Wakati Liverpool wamechoka kutoka na kupress, kasi yake na kulazimisha kutaisumbua Liverpool.

Upande mwingine wa wachezaji watakaochangia matokeo haya ni kasi ya Hazard dhidi ya kasi ya Mane. Timu itakayofikisha vyema mpira kwa yeyote kati yao itanufaika. Bahati nzuri Hazard anajua kucheza dhidi ya Liverpool huku Mane akifahamu namna ya kuziua klabu kubwa. Nyufa dhidi yao hazitakiwi kwani watamoboa ukuta.

Lakini kuna kipenzi cha Klopp, anaitwa Firmino. Wengi wanasahau sana ubora wake na wanapuuza. Firmino tangu kuongezeka kwa Mane imemfanya kuwa mchezaji hatari zaidi kwa sababu anasahaulika sana. Lakini pia ni moja ya viungo nadra sana anayeweza kucheza eneo lote la mbele kwa ufasaha huku akikaba pia.

Huyu mpaka sasa ndiye anaongoza EPL kwa kutengeneza nafasi kwenye maeneo ya wazi, huku pia ndiye mshambuliaji aliyekaba zaidi. Anapenda kucheza jirani na mabeki naa miguu yake ni myepesi sana. Kante anatakiwa kulinda nyendo zake huyu.

Kama kuna mchezaji anayeweza kuwaumiza Liverpool basi ni Coutinho, mpaka pale atakapojua namna ya kuchagua muda upi apige shuti. Conte muue Henderson uifunge Liverpool na inawezekana hili. Klopp anza na Sturridge, Firmino awe huru, hapa hata Mane atakuwa huru zaidi.

Kama unabet, hakuna sare hapa.

Ahsanteni

Nicasius Nicholaus Agwanda (Coutinho Suso)

Niffolow Instagram @agwandanic

No comments

Powered by Blogger.