KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : TATHMINI YA WAPENDA SOKA KUELEKEA MECHI YA LEO CHELSEA VS LIVERPOOL

Ligi kuu ya soka Nchini England Itaendelea leo Ijumaa kwa mechi moja tu kupigwa katika dimba la Stamford Bridge (Darajani).
Mechi inayotarajiwa kaanza saa 4 kamili Usiku kwa saa za hapa nyumbani.

KIJIWENI leo imetazamwa mechi hii na kila mmoja alikua na lake la kuandika kupitia Group page ya Kundi katika mtandao wa Whatsapp.




Ameandika Sylvester Mateso

Ukiangalia viwango vya timu zote basi ni wazi patachimbika.. chelsea hajapoteza game, na morali waliyonayo katika kusaka ushindi ndio silaha yao kubwa.. hawa majogoo si wa kuaminika sana kwa sababu form yao leo inapanda kesho inashuka, japokuwa kocha wao ana mbinu nyingi za kusaka ushindi....

Sioni nafasi ya liverpool kutawala kiungo... uwepo wa Kante na Matic ni mwiba kwa wapinzani, lakini pia silaha kubwa ya Liver pool ni kushambulia kwa kasi, hapa wanahitaji ubora wa Sadio Mane na Firminho kuliko chochote...

Joel Matip kwa Costa, hapa kuna shida.. akili ya ziada yahitajika kumkaba huyu bwana mana anakukera kitabia afu pia anakukera kwa kukufunga..

Utabiri wangu ni chelsea 3 liverpool 2

AMEANDIKA Eric Temu

Kasi ya liverpool ndio inayoonekana kuwapa ushindi  wa mezani liverpool, wachezaji wenye kasi kama Mane, Firminho na Coutinho hawa naona kama silaha kubwa ya counter attack huku ukizingatia beki za chelsea zilivyo

Utabiri wangu: Chelsea 1-2 Liverpool

AMEANDIKA Festo Kalawa (Fes Arsenal)

Daah midadi ya makocha kiburudisho cha mechii
Usikose kuiona miwani ya Klop ikianguka
Usikose kuona kumbatio la KONTE kwa yeyote atakaejitokeza mbele yakeee

Mechi 50/50
utabiri wangu: Chelsea 1-2 Liverpool

AMEANDIKA Elia Ruben

 Naamini utakuwa mchezo mzuri. Liverpool wanazidi kubadilika kila kukicha. Wijnaldum na Henderson wapo imara.  Utakuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili.

Utabiri wangu: Sare ya bao 2-2

AMEANDIKA Nelson Rukiza (Sir Nelly)

Courtois simama kwenye nafasi yako Coutinho mda si mrefu anapiga shuti nje ya 18...

Ni wazi kwamba hakuna asiyejua mbio fupi za mita 100 ambazo Usain Bolt anajivunia basi ndio zile winger na forwad zenye njaa za Liverpool zilizomuangamiza Leicester City.

Binafsi wengi tulijua kua msimu huu Liverpool watapotea lakini ile ari waliyoonyesha kwa Leicester Citt naweza sema ile ndio Liverpool tuliyokua tukiitazamia kuiona chini ya Klopp, sina shaka na mbinu zake ila kujiamini kwa kikosi kizima kinaleta muamsho na msisimko....

leo usiku ni siku ambayo mtoto huwezi mtuma dukani esp kama unakaa kigamboni penLiverpooi.

Nikianza na wenyeji Chelsea ikiwa chini ya kocha mwenye hiba ya amsha amsha Antonio Conte wamecheza michezo minne na kushinda mitatu huku wakilazimishwa sare mara moja na Swansea sare ambayo ilitokana na makosa madogo ya bsare

Terry nje, Luiz ndani Chelsea watajivunia uwepo wake huku akiwa na kariba ya kupandisha timu na uwezo mzuri wa kuokoa mipira iliyokufa namuamini sana Luiz ambaye mbele yake yupo mdogo wake KANTE asiyetabasamu wakati wa mchezo uwanjani huku akisaidiwa na Matic, naamini Kante atakua Backup ya Luiz kama ikitokea atapandisha mashabulizi itambidi arudi nyuma kuziba ukuta....

Shikamoo Fabregas najua sijakuacha ila Sub yako ya dk.70 itakua yenye manufaa pale utakaleta nguvu mpya..
Hazard na Costa naamini wataendeleza kazi nzuri waliyoianza toka siku ya kwanza...nina kila sababu ya kusema Kante hakikisha Mtu anapita mpira unabaki...

Liverpool wanarudi na morale mpya ya ushindi mnono kwa Leicester a huku beki wao Lovren akirejesha ukuta mpana....sina shaka kabisa na viungo washambuliaji maana wakitulia basi ntaziona zile za kampa kampa tena za Leicester....

Beki za Liver zinatakiwa kua makini na Diego costa ambaye utulivu wake unakua kila siku huku Hazard akiendeleza mbio za mwenge hivyo utulivu wa mabeki ni muhimu kwa mabeki wote maana chochote chaweza tokea tukaskia Penati na kadi nyekundu.

Viungo bora ndio watakao amua mchezo wa leo maana watapunguza mashambulizi.

Ikumbukwe kua mechi ipo darajani
Utabiri wangu ni : Chelsea 2-0 Liverpool

AMEANDIKA Hamad Mabula

Naiona Chelsea ya Konte ikiingia kwenye mchezo wa Leo ikiwa, na sababu zote za kushinda, ipo nyumbani, Luiz sehemu ya ulinzi, Kante na matic kwenye kiungo na Costa sehemu ya ushambuliaji..

Japo tabia ya Luiz kupenda kupanda sana na makosa madogo madogo yanaweza kuwapa faida Liverpool hasa tukizingatia uwepo wa safu ya ushambuliaji yenye wachezaji wenye kasi na udambwi dambwi kama Mane, firminho na Coutinho hasa kwenye mashambulizi ya kushtukiza!

  Zaidi ya yote ni burudani na ile midadi nje ya uwanja kutoka kwa makocha wa timu zote mbili.

Utabiri wangu : Chelsea 3 Liverpool 1

AMEANDIKA Edo DC

Kwanza kabisa nawapa Ushindi Chelsea katika mechi hii na hoja zangu zote nitazielekeza kutetea ushindi kwa Chelsea leo.

 REKODI YA KUTOFUNGWA NYUMBANI

Moja ya sababu zinazomfanya Antonio Conte aheshimike duniani ni uwezo wa timu yoyote anayoifundisha kutofungika ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani.

Ameshacheza mechi 21 za ligi bila kupoteza akiwa katika uwanja wa nyumbani na hii ni tangu alipokua Juventus na hajapoteza mchezo wowote Katika ligi tangu January 2013 Juventus walipofungwa na Sampdoria akishinda mara 30.

UJENZI WA TIMU

Ligi kuu ya England msimu huu inanogeshwa na uwepo wa makocha wahamasishaji anachomtofautisha Conte na hao wengine ni uwezo wake wa kutengeneza timu kila idara.

Chelsea hii ya sasa bao linaweza kupatikana kutoka kwa mchezaji yeyote ndo mana katika mchezo uliopita wachezaji wote isipokua kipa walikua shots (walijaribu kufunga) hata kama hazikulenga goli.

BEKI NA VIUNGO IMARA

Ukiacha beki za Arsenal na Leicester City ambazo zilishindwa kuikabili kasi ya ushambuliaji ya Liverpool hali ni tofauti kwa safu ya Ulinzi ya Chelsea ikiongozwa na David Luiz na Gary Cahill, Branslav Ivanovic na Cesar Azpilicueta bado mabeki hawa watu wanalindwa na viungo imara Nemanja Matic na N'golo Kante au pengine hata Obi Mikel na mwenzie Fabregas.

Ijapokua washambuliaji wa Liverpool wana kasi mno lakini sioni namna watakavyoweza kuupita ukuta huu na kuleta madhara kama yale ya Emirates au Anfield katika mechi iliyopita.

WASHAMBULIAJI WENYE UCHU WA MABAO

Diego Costa,Eden Hazard,Willian na Oscar hawa watu wanaenda kuikabili safu ya ulinzi ya Liverpool ambayo imekua na makosa kibao mpaka kupelekea kwa kiungo James Milner kupelekwa kucheza beki ya pembeni.

Kwa upande wa Liverpool ninachokiona zaidi ni ile kasi ya kutengeneza mashambulizi hasa ya kutumia mfumo wa kustukiza na wakati mwingine pasi fupi fupi ambazo zinatengenezwa timu ikiwa kwenye kasi hii ni silaha tosha sana kwao kama watafanikiwa kupata bao la mapemazaidi.

Historia pia inawapa neema Liverpool katika uwanja wa Stamford Bridge kwani wamekua wkishinda sana katika uwanja huo Liverpool wameshinda mara 4 na kupoteza mara 2 tu huku sare ikowa ni mara 3 katika michezo ya hivi karibuni.

All in all nategemea mchezo mzuri sana leo nadhani tutashuhudia magoli mengi pia yakifungwa.

NATABIRI : Chelsea 3-2 Liverpool


AMEANDIKA Zein 

Kawaida mechi kubwa kama hizi zinakuwa ni zaina yake kutokana na wachezaji kuwa na tention kubwa...!!! Uchambuzi wangu ni kama ifuatavyo ;

Nikianza na wenyeji wa mchezo, Chelsea wakiwa na kocha mpya Antonio Cante ambaye mfumo wake ni wakukaba kwa asilimia 75% anaweza kuwazuia liverpool, Chelsea wana defence nzuri ijapokuwa defence yao imeonyesha mapungufu katika mechi mbili zilizopita, vile vile Chelsea wana safu zuri ya ushambuliaji kitu ambacho kitaweza kuwasumbua Liverpool.

Mpaka sasa ukingalia Costa na Hazard wameonyesha kuelewana na kuwapa shida wapinzani, konte ameonyesha kuli miliki dimba vizuri katika kuharibu mbinu za wapinzani. Ushauri kwa chelsea leo wamuanzishe Fabrigas wampumzishe Oscar....maana Fabrigas ameonyesha kutoa pasi za mwisho nzuri zilizozaa matunda.

Upande wa Liverpool Kocha wao Klop ameonekana kuwa mjanja sana anapokutana na timu kubwa na tangu ameingia Epl kuiongoza liverpool karibu timu kubwa zote amezifunga, vile vile Liverpool wameonekana kuimarika kila baada ya game hasa baada ya wachezaji wake tegemezi kupona kwa asilimia 100%.

Klopp ameijenga Liverpool katika kufanya attack nyingi ambazo ziitaifanya timu kushinda, huku akijaribu kuimarisha beki yake inayoruhusu magoli ya kizembe.

Chelsea wapaswa kuwachunga Firmino na Mane maana wameonekana kuonyesha makali tangu ligi kuanza vile vile wasimsahau Coutinho ambaye aliwaadhibu kabla ya Mourinho hajaondoka.

Liverpool wanapaswa kuwa makini kwenye kulinda na kutokukubali kuruhusu magoli ya haraka na kizembe.

Utabiri wangu
Chelsea 1-3 Liverpool
Chelsea 1-1 Liverpool
Chelsea 1-0 Liverpool

KWA LEO NI HAYA TU KUTOKA KIJIWENI TUKUTANE SIKU NYINGINE.

Sâš½KA LETU | JAMII YETU

No comments

Powered by Blogger.