YANGA YAMALIZA UKIMATAIFA KWA KUCHAPWA NA TP MAZEMBE

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wamemaliza uwakilishi wao katika michuano ya kimataifa kwa kichapo cha bao 3-1 toka kwa TP Mazembe ya Congo.



Yanga ambayo ilisafiri mpaka Congo kuwavaa mabingwa hao wa Afrika ilijikuta ikichapwa bao hizo 3-1 katika mchezo wa kukamilisha ratiba tu katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mpaka mapumziko tayari Yanga walishafungwa bao 1-0 huku wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Andrew Vicent kulimwa kadi nyekundu huku goli la Mazembe likifungwa na Boling Jonathan.

Kipindi cha pili Mazembe waliongeza kasi wakikosa mabao mengi huku wakifanikiwa kufunga mabao mawili kupitia kwa Rainford Kalaba dakika ya 56 na 64 kabla ya Amiss Tambwe hajafunga bao la kufutia machozi kwa Yanga.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga wamemaliza uwakilishi wao katika michuano ya kimataifa na watarejea kwaajili ya ligi kuu Tanzania bara.

No comments

Powered by Blogger.