TAIFA STARS NA NIGERIA SASA NI SEPTEMBA 3,MKWASA KUTANGAZA KIKOSI KESHO
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Nigeria (NFA), limesogeza mbele kwa siku moja mchezo kati ya timu ya taifa ya
Nigeria ‘The Super Eagles’ na Tanzania ‘Taifa Stars’ ambako sasa utafanyika
Septemba 3, 2016 badala ya Septemba 2, 2016 iliyotangazwa awali.
Na Kocha Mkuu wa Taifa Stars,
Charles Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho atakiandaa
maalumu kwa mchezo huo. Mkwasa amesema kwamba anatarajia kuita wachezaji 20
ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo.
“Kutakuwa na mabadiliko kidogo
katika kikosi nitakachotangaza. Kwanza watakuwa wachezaji 20 badala ya 24, pili
wachezaji ambao nitawachukua ni tofauti tofauti maana wengine kwa sasa ni
majeruhi,” amesema Mkwasa.
Mchezo huo ni wa kukamilisha
ratiba katika kundi G baada ya Misri kukata tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa
ya Afrika, fainali zitakazofanyika Gabon, mwakani. Katika kundi hilo, Chad
ilijitoa hivyo kuathiri mbio za ushindani wa nafasi hiyo kwa timu za Tanzania
na Nigeria.
No comments