SERENGETI BOYS KUPIGA KAMBI NYINGINE NJE YA NCHI TAYARI KUWAVAA CONGO
Baada ya kutekeleza ahadi ya
mwanzo ya kuipeleka Madagascar kwa ajili ya kambi ya kuivaa Afrika Kusini
‘Amajimbos’, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amepanga kutekeleza ahadi yake nyingine kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania
ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwenye kambi tulivu,
ikiwezekana nje ya nchi.
Rais Malinzi aliahidi na
kutekeleza ahadi yake kuipeleka Madagascar Serengeti Boys baada ya kuitoa
Shelisheli katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika
Madagascar, mwakani. Kadhalika aliahidi kuipeleka timu hiyo nje ya nchi ambayo
hata hivyo haijateuliwa baada ya kuindoa Afrika Kusini. Ameahidi kambi hiyo
itaanza Septemba mosi, mwaka huu.
Serengeti Boys ilipiga kambi
Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa wiki moja kabla ya kuhamia Hoteli ya Urban
Rose, katikati ya jiji la Dar es Salaam ambako ilivunjwa kwa muda jana Agosti
22, 2016 ambako vijana wamekwenda makwao kusalimia ndugu zao na itaitwa
mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya nje ya nchi.
Serengeti Boys imebakiwa na
mtihani mmoja kufuzu kucheza fainali hizo kwa kucheza na Congo – Brazaville na
mchezo wa kwanza utafanyika Dar es Salaam, Septemba 18, 2016 kabla ya kurudiana
Septemba 30, 2016, Oktoba 1 au Oktoba 2, 2016.
TFF imejipanga kwa ajili ya kambi
hiyo, na kinachosubiriwa kwa sasa ni mapendekezo ya makocha ili shirikisho
itekeleze hatua hiyo ya kambi ya utulivu.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi
Mweusi amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila
timu nitajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.
No comments