YANGA YAANZA KUTETEA UBINGWA KWA USHINDI, MBEYA CITY YAIMALIZA TOTO KWAO.

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga leo wameanza harakati za kutetea ubingwa wao kwa kuizamisha African Lyon kwa bao 3-0.


Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini ulikua wa kwanza katika ligi kwa Yanga baada ya kutolewa katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ukiwa pia ni mchezo wa pili kwa African Lyon.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke,Simon Msuva na Juma Mahadhi

Alex Sanga kutoka Mwanza anaripoti kwamba Mbeya City imeweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Toto Africans ya Mwanza katika dimba la CCM Kirumba.

Mpaka Mapumziko tayari Mbeya City walishakua mbele kwa bao hilo moja likifungwa na Haruna Shamte aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Toto Mussa Kirungi na kutinga wavuni goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.


No comments

Powered by Blogger.