MIRABA SABA YA CHARDBOY77 KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND.

Na Richard Leonce
Karibu tena kwenye miraba saba, tuangalie mambo mbalimbali ya kitakwimu kwenye michezo ya Ligi kuu ya England iliyochezwa Agosti 27.


1. Kuna kitu kwenye magoli ya James Milner, jana aliifungia Liverpool kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham, ilikua mara ya 42 kufunga, kisha timu aliyoifungia isipoteze mchezo. Ni Darius Vassel pekee aliyeweza kufanya hivyo mara 46 ndiye aliye juu ya Milner.
Kabla ya goli la Tottenham jana, walikua hawajawafunga Liverpool bao lolote la ligi kuu kwenye uwanja wa White Hart Lane tangu November  2012 alipofunga Gareth Bale.

Liverpool sasa wameruhusu wavu wao kutikiswa kwenye michezo yao nane mfululizo ya ligi kuu walipocheza ugenini..
Mchezo wa Tottenham V Liverpool na Everton V Newcastle ndiyo michezo iliyozalisha penati nyingi zaidi. Imezalisha 20 kila mmoja.

2. Kocha wa chelsea Antonio Conte sasa amepita kwenye michezo 30 mfululizo ya ligi kuu bila kuona kichapo. Ameshinda 28 na kutoa sare 2.
Diego Costa amehusika kwenye goli katika michezo mitano mfululizo iliyopita ambayo ameichezea Chelsea kwenye ligi kuu. Amefunga mabao 3 na pasi 2 za mabao.
Burnley wao hawajawahi kupata ushindi wowote wa ligi kuu kwenye uwanja wa Stanford Bridge tangu 1971.
Goli la jana la Victor Moses kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Burnley lilikua lakwanza kwake kuifungia Chelsea kwenye ligi kuu tangu 2012.

3. Sare ya 1-1 dhidi ya Bournemouth inamaanisha Crystal Palace wamekosa ushindi katika michezo 20 kati ya 22 ya ligi kuu waliyocheza mfululizo. Wamepata sare 6, vichapo 14.
Yohan Cabaye amekosa penalt mbili mfululizo za ligi kuu alizopiga. Kabla ya hapo alifunga nne fululizo.
Golikipa wa Bournemouth Artur Boruc ameokoa michomo mitatu mfululizo ya penalt aliyokutana nayo wakati Mike Dean akiendelea kua mwamuzi aliyetoa penalt nyingi zaidi tangu msimu wa 2015/16. Ametoa penalt 17.

4. Golikipa wa Stoke Shay Given alijifunga na kuwazawadia Everton ushindi wa bao 1-0. Hii siyo mara ya kwanza kujifunga, ni mara ya pili kwake. Ajabu ni kwamba mara zote mbili zimekua dhidi ya Everton, mara ya kwanza ilikua Oktoba 2007.
Stoke wameshapigiwa penalt kwenye michezo miwili kati ya mitatu ya ligi kuu waliyocheza mpaka sasa msimu huu.
Mpaka sasa Everton hawajapoteza mchezo katika michezo mitano iliyopita waliyocheza nyumbani Goodison Park, kabla ya hapo walipata ushindi mmoja tu katika mechi 9.

5. Ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea walioupata Leicester ulikua ni ushindi wa 100 wa kocha wao Claudio Ranieri kweye ligi kuu ya England.
Jamie Vardy aliifungia Leicester goli lake la 30 la ligi kuu. Ni mchezaji wa tatu kufanya hivyo nyuma ya Muzzy Izzet na Emile Heskey ambao wote waliifungia Leicester mabao 33

Leicester hawajafungwa na Swansea katika michezo 12 iliyopita ambayo wamecheza nyumbani, wakati Riyard Mahrez yeye amekosa penalt tatu kati yanne zilizopita ambazo alichukua jukumu la kupiga.

6. Jermain Defoe ni mzuri sana awapo mbali na nyumbani amefunga mabao 10 kwenye michezo 10 ya ugenini ya ligi kuu.
Alexis Sanchez amekutana na Watford mara 3 kwenye ligi kuu na mara zote amewafunga.
Mara ya mwisho Watford kufungwa mabao matatu kipindi cha kwanza ilikua mwaka 2007 walipokutana na QPR.
Tangu msimu wa 2015/16 Watford wamepigiwa penalt 9, ni Norwich pekee waliopo juu yao wakiwa wamepigiwa penalt 10.
Mpaka sasa Watford wametumia wachezaji 21 kutoka mataifa 17 tofauti msimu huu.

7. Arsenal walipiga mashuti saba yaliyolenga lango kwenye ushindi wa 1-3 dhidi ya Watford, sita kati ya hayo waliyapiga kipindi cha kwanza.
Watford wao walipiga mashuti 6 kwenye mchezo huo na yote waliyapiga kipindi cha pili.
Idadi ya mashuti 6 ya Watford ni sawa na jumla ya mashuti yote waliyopiga kwenye michezo miwili ya kwanza, walipiga mashuti matatu kwenye kila mchezo.

Marcus Rashford sasa amefunga magoli 6 kwenye michezo 12 ya ligi kuu.
Man UTD wameshinda michezo mitatu ya ufunguzi kwa mara ya kwanza tangu msimu 2011/12.
Hull City ndiyo timu iliyopigiwa mashuti mengi zaidi msimu huu, Mpaka sasa wamekutana na makombora 70 yakielekea upande wao, lakini wamefungwa mabao mawili tu.
Manchester UTD wamewahi kufunga dakika za 90 mara 18 katika ligi kuu.

No comments

Powered by Blogger.